Home Kitaifa KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE UWEKEZAJI YATEMBELEA UJENZI WA MELI YA MV...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE UWEKEZAJI YATEMBELEA UJENZI WA MELI YA MV MWANZA HAPA KAZI TU

Kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma(PIC imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa Ujenzi wa Meli ya Mv Mwanza Hapa Kazi Tu uliyofikia asilimia 80 ya Ujenzi Wake ambao utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 109 hadi itakpokamilika mwezi Agosti mwaka huu kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya usafiri katika Ziwa Victoria.

Rai hiyo imetolewa Jijini Mwanza na Mwenyekiti wa kamati hiyo mheshimiwa.Jerry Silaa (mbunge) mara baada kutembelea na kugagua Ujenzi wa Meli mpya na ya kisasa ya Mv Mwanza hapa Kazi tu

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa huduma za meli (MSCL) Jenelali msitafu John Mbungo amesema, bodi hiyo itahakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi na kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika.

Meli ya Mv Mwanza hapa kazi tu baada ya kukamilika itafanya shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo ndani ya Ziwa Victoria kati ya mkoa wa Mwanza,Kagera na Mara pia na kwa nchi ya Kenya na Uganda.

Katika hatua nyingine kamati hiyo imesisitiza uwepo wa matumizi bora na sahihi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa utekelezaji wa miradi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!