Home Kitaifa MAKANGULA: SITOWEZA KUWAVUMILIA VIONGOZI AMBAO HAWATEKELEZI WAJIBU WAO

MAKANGULA: SITOWEZA KUWAVUMILIA VIONGOZI AMBAO HAWATEKELEZI WAJIBU WAO

Uongozi wa Umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Ubungo (KAMATI YA UTEKELEZAJI) chini ya Mwenyekiti wake shadrack Makangula Leo umeanza ziara yake rasmi ya kutembelea kata ya MBURAHATI NA MAKURUMLA kwa lengo la kwenda kukagua Uhai wa Jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Ubungo kwa ngazi ya kata zote 14.

Aidha Makangula amewataka viongozi wa jumuiya hiyo kutekeleza majukumu yao na kuacha kufanya kazi Kwa mazoea ” upo wajibu mkubwa kwa viongozi wa kata kuhakikisha jumuiya Kwa ngazi zote kuanzia kata, matawi Hadi kwenye mashina zinakuwa hai nyakati zote, sitoweza kuwavumilia viongozi ambao hawatekelezi wajibu wao kila mtu alijaza fomu kulingana na upeo wake bila ya kusulutishwa na mtu hivyo utashi ule ule tuliokuwa nao kipindi Cha chaguzi za ndani za Chama ndio utashi ule ule tuutumie katika kutekeleza wajibu wetu

Hata hivyo Makangula amewataka vingozi kutengeneza mahusiano mazuri na makundi mbalimbali yaliyopo katika maeneo yao, kushiriki katika shughuli za kijamii na kubuni miradi mbalimbali itakayichochea ustawi wa Jumuiya na kuondokana na dhana Tegemezi za mara Kwa mara ” tupo kwenye hizi nafasi kuwasaidia vijana wenzetu twendeni tukawasaidie sisi ndio kimbilio lao

Vile vile amewataka viongozi wa UVCCM wanapoomba fedha kwa wadau, wahisani, mataasi, Makampuni na Mashirika wahakikishe “kile kinachopatikana au mnachopewa kinaenda kufanya shughuli husika na si vinginevyo hii itaendelea kuiletea heshima jumuhiya yetu ya UVCCM na Imani kubwa kwa wadau kiujumla” alisema Makangula

Sambamba na hayo amewataka vijana kutembelea miradi yote inayotekelezwa na serikali na kuangalia fursa mbalimbali zilizopo katika miradi hiyo Ili ikawe sehemu ya kuwasaidia vijana wetu kupata fursa za ajiri za muda mfupi (short term) na muda mrefu (Long term) kuweza kuwapa vijana wa maeneo yao fursa hizo. Tunatambua serikali yetu ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imeendelea kupambana na changamoto za ajira Kwa vijana Kwa kubuni programu mbali mbali kama program ya BBT (Building a Better Tomorrow) wa kuwasaidia vijana kushiriki katika fursa ya kilimo nk hivyo na sisi ni wajibu wetu kuisaidia serikali kuja na mawazo mbadala ya takayochochea ongezeko la fursa Kwa vijana wetu ” alisema Makangula

Aidha amewataka vijana kutumia fursa za mikopo ya halmashauri ili kuweza kuwainua kiuchumi kama ilivyodhamira njema ya serikali lakini pia ni wajibu wao Kwa pamoja kuhakikisha fedha mnazokopeshwa mnazirejesha Ili na vijana wenzenu wengine waweze kupata nafasi ya kukopeshwa mikopo hiyo ” hatutovumilia au kuvioena haya vikundi vilivyopewa fedha lakini havirudishi fedha hizo manispaa, sababu matarajio yetu tunataka kuona vijana wetu wakiendelea kufaidika na fursa hiyo ” alifafanua Makangula.

Aidha Makangula amewataka maafisa maendeleo wa ngazi zote kuanzia wilaya na kata kuweka utaratibu wa kutembelea vikundi vilivyoko katika maeneo yao mara kwa mara ili kujua maendeleo na mienendo ya vikundi hivyo vilivyopata mikopo na changamoto ambazo zinazosababisha kutokurejesha mikopo hiyo Kwa ujumla.

Kwa upande wake katibu wa UVCCM wilaya ya Ubungo Nehemia Philemon amewashauri vijana wote wahakikishe wanaanda semina za mafunzo ya ujasiriamali ili kuweza kuwainua kiuchumi na kimaendeleo.

Nae afisa kutoka idara ya maendeleo ya Jamii wilaya ya ubungo (Ally) ameshauri vijana kuunda makundi ya watu wanaofaamiana na kuelewana vyema kuanzia watu watano Ili kuweza kupata fursa hiyo ya mikopo.

Viongozi hao walitembelea makundi maalum ya vijana hususani wanaojishughulisha na udereva wa boda boda na mama lishe Kwa lengo la kujua changamoto zao pamoja na soko la MBURAHATI, vikundi vilivyopata mikopo ya 4% na kituo Cha afya Cha Makurumla ambao ujenzi wake utakapo kamilika unatarajia kutumia kiasi Cha million 300.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!