Home Afya KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA UTEKELEZAJI MIRADI YA AFYA RRH-IRINGA

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA UTEKELEZAJI MIRADI YA AFYA RRH-IRINGA

Na. Majid Abdulkarim, Iringa

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Afya na Maswala ya Ukimwi imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkoani Iringa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo ambapo amesema kuwa miradi hiyo inaendana na thamani ya fedha iliyotolewa.

“Wabunge tumejionea kwa macho na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi katika hospitali hii miradi yote tuliona inafanya kazi na imekamilika, hivyo inaendana na thamani ya fedha iliyo tumika”, ameeleza Mhe. Nyongo.

Pia amewatia moyo watumishi wa hospitali hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na uzalendo ili kuhudumia Watanzania.

Aidha ameipongeza Serikali kupitia Wizra ya Afya kwa kazi nzuri ya kuhakikisha inafika asilimia 52 ambayo ni sawa na nusu ya watanzania wote waliopata chanjo ya Uviko-19.

Ametoa wito kwa wadau wa maendeleo nchini kujitokeza kushiriki na kufadhiri miradi ya maendeleo katika sekta ya afya.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu ametoa rai kwa watumishi wa afya kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, weledi na viapo vya taaluma zao ili kuleta ufanisi mzuri katika kuhudumia wananchi.

Mhe. Ummy amesema kuwa utekelezaji wa miradi na huduma nzuri walizoziona katika hospitali hiyo ni taswira ya hospitali zote za mikoa nchini.

Mhe. Ummy amesema kuwa baada ya kukamilika miradi iliyokuwa ikitekelezwa katika hospitali hiyo sasa ina uwezo wa kulaza wagonjwa maututi zaidi ya 12 tofauti na ilivyo kuwa awali.

Amesema kwa upande wa wagonjwa dharura mpaka sasa hospitali hiyo inauwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa 500 kwa wakati mmoja.

“Na hayo ni matokeo ya kazi nzuri aliyofanya Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan”, ameeleza Mhe. Ummy

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!