Home Kitaifa Maelfu yakipokea Kwa Shangwe Kituo cha Kisasa cha Redio Rufiji

Maelfu yakipokea Kwa Shangwe Kituo cha Kisasa cha Redio Rufiji

Na John Mapepele

Maelfu ya Wananchi wa Ikwiriri- Rufiji na vitongoji vyake usiku huu wamefurika katika Tamasha la uzinduzi wa
Rufiji FM – Raha ya Pwani Redio pendwa kwa watu wote.

Kituo hicho cha Redio kimezinduliwa jioni ya Machi 12, 2023 na Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Rufiji, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa kinakuwa miongoni mwa vituo vichache nchini kinatumia teknolojia ya kisasa kabisa.

Mhe. Mchengerwa amesema kituo hicho kitajikita katika kuandaa maudhui yanayozingatia maadili ya kitanzania.

Tunaamini kituo chetu kutoa huduma bora kabisa katika kuwahabarisha, kuwaburudisha na kuwaelemisha Warufiji, Wanapwani na watanzania kwa ujumla.

Tunamshukuru Mhe, Mchengerwa kwa kutuletea kituo hiki cha Redio ambacho tumekipokea kwa mikono miwili, kitatusaidia Sana katika masuala ya kijamii” amesema Amri Said mkazi wa Ikwiriri

Aidha, Mhe Mchengerwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi katika huduma za jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!