Na Bwanku M Bwanku.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Ndugu Sophia Mjema amesisitiza kuwa wanaCCM kamwe wasikubali kunyamaza bali waendelee kusemea haya makubwa na mazuri yote yanayofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mjema ameyasema hayo Jana Alhamisi Machi 02, 2023 kwenye mwendelezo wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo na Sekretarieti yake kwenye wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
“Tunae Mama (Rais Samia) anayetujali, anayetuletea maendeleo na hatuwezi kunyamaza. Nani atanyamaza kama Serikali yake inampa mtoto wake elimu bila kulipa, utanyamaza kama mkeo ameenda hospitali amepata sehemu nzuri ya kujifungua utanyamaza? utanyamaza wakati mbolea imeshushwa tulikuwa tunanunua Laki 1 na 50 hadi 60 leo kwasababu ya ruzuku aliyotoa Rais Samia kwenye mbolea tunanunua mbolea kwa Elfu 70.” Alihoji Mjema.
Mwenezi Mjema ameendelea kusema CCM itaendelea kumuunga mkono Rais Samia na kumsemea kwasababu CCM ndiyo Chama kilichoshika Dola na kinachoongoza Serikali na kina jukumu la kusema haya.