Home Kitaifa SHIRIKA LA TMFD LABAINI WATOTO KUTUMIKISHWA KWENYE MIALO

SHIRIKA LA TMFD LABAINI WATOTO KUTUMIKISHWA KWENYE MIALO

Kwenye mialo mingi ya uvuvi kuna suala la ajira za watoto kwani wazazi wamegeuza watoto kuwa ni sehemu ya nguvu kazi ya utendaji kazi za uchakataji, jambo ambalo sio sawa Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TMFD kwenye mkutano wa NGOs Mkoa wa Mwanza

Mkurugenzi wa shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisheries Development Bwana Edwin Soko amesema kwenye sekta ya uvuvi kuna changamoto ya ajira za watoto.

Soko amesema hayo kwenye mkutano wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoa wa Mwanza uliofanyika leo Jijini Mwanza.

Soko amesema kuwa kuna baadhi ya maeneo ya uvuvi watoto wadogo wamekuwa wakitumika kwenye shughuli za uchakataji kwa kushiriki kama sehemu ya kifamilia au ajira

Soko ameongeza kuwa, kwa sasa shirika la TMDF lina mpango wa kufanya uchechemuzi wa athari za ajira za watoto kwenye sekta ya uvuvi

“Kwa sasa shirika la TMFD linapanga kufanya tafiti kwenye sekta ya uvuvi ili kubaini ukubwa wa tatizo la ajira za watoto kwenye mnyororo wa thamani ya mazao ya uvuvi “ Mkurugenzi wa TMFD Edwin Soko

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!