Home Kitaifa SERIKALI YATOA KIBALI KWA KAMPUNI YA EACOP KUANZA UJENZI WA BOMBA LA...

SERIKALI YATOA KIBALI KWA KAMPUNI YA EACOP KUANZA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA AFRIKA MASHARIKI

Na Magrethy Katengu

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imekabidhi kibali cha ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki kwa kampuni ya EACOP Tanzania LTD kwaajili ya kuanza Ujenzi wa Bomba hilo kutoka Mtukula Nchini Uganda hadi Chongoreani Mkoani Tanga.

Akizungumza Katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam Waziri Wa Nishati Januari Makamba amesema kuwa mchakato wa kukabidhi kibali hicho umezingatia masuala ya utunzaji wa mazingira pamoja na utafiti uliofanyika kwa kina .

Hata hivyo amefafanua kuwa kumekuwa na uvumi wa maneno mengi katika Mataifa jirani kusema kuwa Tanzania haiwezi kuendesha mradi Mkubwa kama huu sisi tumeyakataa maneno yao Dkt Rais Samia Suluhu Hassani amekataa ndiyo maana Leo Dunia nzima kupitia vyombo vya habari wanashuhudia kibali cha Ujenzi kikitolewa na Serikali imejidhatiti hakuna kitakachoshindikana

Sanjari na hayo amesema Mikoa yote minane ambapo bomba hilo litapita hakuna atakayelamu kwani tayari mradi umeanza kutekelezwa kwa kulipa fidia kwa wakati hivyo kaya zaidi ya 9800 wameshalipwa fidia.

Tayari tumelipa fidia shilingi bilioni 29, na mradi huu umeanza kutekelezwa katika baadhi ya maeneo, mfano kununua vifaa, kuanza ujenzi wa vituo vya kuhifadhia mafuta Mkoani Tanga. kwa hiyo tunatarajia mradi huu ulete ajira nyingi za moja kwa moja lakini pia ajira za kutoa huduma kama vile hoteli, hivyo Watanzania wachangamkie fursa hizi” amesema Waziri Makamba.

Hata hivyo ameitaka Malaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) ambayo imepewa asilimia 15 ya usimamizi wa mradi huo kwenye kampuni ya EACOP kuhakikisha inatangaza fursa zilizopo pamoja na kusimamia ipasavyo sheria ya Local Content kwa kuhakikisha wazawa wanapata fursa mbalimbali zitokanazo na mradi huo na kuhakikisha wazawa wanafaidika na mradi.

Awali akizungumza Katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji EWURA Dkt James Andilile Mamlaka hiyo imepewa jukumu ambalo watahajikisha wanatekekekele vizuri maagizo waliyopewa.

“Kampuni ya EACOP imepewa zabuni hiyo kutokana na kukidhi masharti ya kimkataba ikiwemo kuzingatia masuala ya utunzaji wa mazingira, Athari za kibinadamu, pamoja na uwezo wa kitaalamu na kifedha kwa ajili ya kutekeleza mradi”amesema Mkurugenzi

Ujenzi huu wa kipande cha kutoka Mtukula hadi Chongoreani Mkoani Tanga una urefu wa kilomita 1147 , sisi kama EWURA tuna matumaini kwamba kampuni ya EACOP TZ itaendelea kuzingatia yote tuliyokubaliana kabla na baada ya ujenzi wa Bomba hili” amesema Dkt Andilile.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa waliohudhurua katika hafla hiyo Mradi huo umepita watahakikisha wanasimamia vema miundombinu ya mradi huo kwa kutumia Jeshi la Akiba katika ulinzi hivyo wameomba Serikali kujenga vituo vya polisi katika vituo vya kuhifadhia mafuta ghafi ili kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo wakati wote wa Ujenzi na baada ya kukamilika.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya EACOP Tanzania ambayo imekabidhiwa Kibali cha ujenzi wa mradi huo Bi. Wendy Brown amesema kuwa Kampuni hiyo iko vizuri katika Ujenzi wa Miundombinu ya kuunganisha Nchi Kwa nchi kibiashara na hiyo watahakikisha wanazingatia makubaliano ya mkataba hadi Mradi kukamilika.

Mradi wa Bomba la Mafuta ghafi ambao umepata Kibali rasmi leo unatekelezwa katika mikoa nane ambayo ni pamoja na Tanga, Manyara, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera, ambapo unatarajiwa kutoa fursa mbalimbali za kiuchumi kwa wananchi waishio Katika mikoa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!