Home Kitaifa MGOGORO MKATABA WAFANYABIASHARA SOKO SM 2000, MKUU WA WILAYA UBUNGO AINGILIA KATI

MGOGORO MKATABA WAFANYABIASHARA SOKO SM 2000, MKUU WA WILAYA UBUNGO AINGILIA KATI

Na Magrethy Katengu

Wafanyabiashara Wamachinga wa soko la Ubungo SM 2000 wanakabiliwa na changamoto sitofahamu baina na Halmashauri yao kuhusu ukarabati wa soko hilo kuambiwa kuandikiana Mkataba ukarabati kisha fedha zao kurudi kwa kufanyabiashara bila kulipa kodi kwa miaka kadhaa .

Wakitoa malalamiko yao kwa i Mkuu wa Wilaya Hashim Komba alipofanya ziara ya kushtukiza Mwenyekiti wa Kamati ya Maboresho soko la SM 2000 Mussa Ndile amesema Halmashauri hiyo iliwaletea Mpango wakarabati Sokon hilo kwa fedha zao na watakaa kwa miaka kadhaa bila kulipa kodi kufidia fedha walizotumia hivyo wameshindwa kuafiki kutokana na hali ya biashara hali ni mbaya watu wengi wamehamia kujenga vibanda katika maeneo yaliyozuiwa na wanalipia elfu Moja kwa siku hawalipi kodi lakini wao waliokubali kukaa ndani katika mazingira magumu wanaambiwa hivyo suala ambalo kwao wanashindwa kuelewa .

Kiukweli hatuelewi Halmashauri hii tulitembelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe Amosi Makala akajionea hali halisi ya soko Wafanyabiashara walio wengi wamehamia maeneo yaliyozuiwa na wamejenga vibanda vya kudumu na Ushuru wanalipia sh 1000 kila siku sisi tumewaomba ufafanuzi wanakaa kimya Mbunge Kitilya Mkumbo alikuja kutembelea akaahidi atashughulikia.

Naye Iddy Mussa Mfanyabiashara amesema Soko ni kubwa hakuna wateja vibanda vimekimbiwa Choo kinavuja maji kuelekea maeneo ya wanakofanyia biashara na vibanda vilivyo wazi vimejaa vinyesi hela ya ushuru tunalipia na ya usafi lakini wanafanya biashara katika maeneo hatarishi kupata magonjwa ya mlipuko hivyo Serikali iliangalie hilo.

Naye Mwanasheria wa Halmashauri ya Ubungo Kissa Mbila amejibu hoja za wafanyabishara kwa kusema waliandaa utaratibu wa namna ya ukarabati wa soko hilo kila mfanyabiashara atakarabati kwa kujenga kwa gharama zake na fedha zao watafanyabiashara pasipo kulipia kodi kwa miaka kadhaa hadi fedha zao zitakavyorudi ndipo watakapoanza kulipa kodi lakini wao hawakuridhia.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hashimu Komba alijibu malalamiko ya Wafanyabiashara hao Kwa kusema Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Wafanyabiashara wanakaa katika mazingira mazuri lakini ameaikitishwa na Halmashauri hiyo kukusanya fedha za ushuru lakini Choo kichafu kinatiririsha maji machafu hivyo ametoa maagizo ndani ya siku mbili gari la Maji taka kutoa maji machafu kabla hajawajibishwa mtu

Aidha amesema kutokana na maelezo aliyoyasikia ameona kumekuwa na hofu baina ya pande mbili lakini kama Wafanyabiashara kama wapo tayari kwa maboresho hakuhitaji kuanzisha Mkataba pasipo kujenga lazima Halmashauri ikae na Wafanyabiashara hao wangee nao lugha nzuri ili Mambo yaende sawa kwani siyo wote wenye uwezo wa kukarabati na lazima ufanyike uhakiki wa Wafanyabiashara wote wasije wakajitokeza wajanja kukarabati kisha kukodisha kwa bei kubwa kwani katika masoko mengi hukuta kuna mtu mmoja kumiliki vibanda zaidi ya kumi na kukodisha kwa gharama kubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!