Home Kitaifa MHE. MAHAWANGA AZINDUA SEMINA MAALUM YA MALEZI KWA WATOTO

MHE. MAHAWANGA AZINDUA SEMINA MAALUM YA MALEZI KWA WATOTO

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Mahawanga Janeth leo ameshiriki kama Mgeni Rasmi katika semina ya Haki na kujitambua kwa watoto iliyoandaliwa na Taasisi ya Andalusia Training Centre na kufanyika katika kituo cha kulea watoto na kutoa mafunzo mbalimbali cha Hatua Children Life skills Training Center kilichopo Ukonga, Dar es Salaam.

Katika Tukio hilo Mhe. Mahawanga ameweza kukabidhi vifaa vya Ofisi zikiwemo Kompyuta, Printer, Vyakula na vifaa mbalimbali vya masomo kwa watoto wakishirikiana na Multazar Miran ambaye ni Afisa Utamaduni na masuala ya Kijamii kutoka Ubalozi wa Iran nchini Tanzania, Ndgu Ejaz Bhalloo kutoka kituo cha Andalusia Training Centre.

Mhe. Mahawanga amempongeza sana Ndgu Ejaz Bhalloo kutokea kituo cha Andalusia Training Centre ambacho amekizindua leo kwa kuandaa tukio hilo la kuwatembelea watoto wakishirikiana na Taasisi mbalimbali ikiwemo Lions Club of Mzizima, Lions Club of Panorama na Bi. Zahra Habib kwa ushirikiano wao katika kufanikisha shughuli hiyo.

Aidha ametoa pongezi kwa Walimu wote katika kituo hicho na kipekee kumpongeza Ndugu Justus August ambaye ni msimamizi mkuu wa kituo hicho na kuahidi kufanya naye kazi kila hatua kuhakikisha kituo hicho kinaendelea na jukumu la kuwalea vyema watoto maana dhamira yake kama kiongozi na mzazi ni kuhakikisha pia watoto wanakuwa katika malezi mazuri na kuwa na manufaa kwa Taifa baadae.

Pia Mhe. Mahawanga amewasisitiza waendelee kumuunga mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan maana ana dhamira nzuri ya kuhakikisha watanzania wote wanapata maendeleo lakini sambamba na kuhakikisha sekta hii ya viwanda inakuwa zaidi Tanzania aidha pia amewataka wanawake kama mabalozi Wazuri kujitokeza na kuunga mkono zoezi la Sensa maana lina umuhimu sana katika kuhakikisha Taifa linapata takwimu sahihi za watanzania ili kutoa mahitaji muhimu ya Maendeleo kulingana na takwimu hizo.

Mwisho ametumia Fursa hiyo kuwatakia Eid-ul-Adha kwa waumini wa dini ya Kiislamu na watanzania wote nakuwaombea baraka za Mwenyezi Mungu ziangaze maisha ya watanzania wote na kutumaini kwamba furaha, amani na mafanikio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!