Home Kitaifa HOSPITALI MPYA ZA WILAYA 135 ZAJENGWA NA RAIS DKT. SAMIA NCHI NZIMA.

HOSPITALI MPYA ZA WILAYA 135 ZAJENGWA NA RAIS DKT. SAMIA NCHI NZIMA.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe, Dkt. Festo J. Dugange amesema hospitali mpya za wilaya 135 zimejengwa nchi nzima katika kipindi cha miaka miwili ya utawala wa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amasema hayo tarehe 05 Februri 2022 mkoani Njombe wakati akieleza utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika maadhimisho ya miaka 46 kuzaliwa kwa CCM kimkoa.

Dkt. Dugange amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameimarisha utoaji wa huduma za afya nchini ambapo amewezesha ujenzi wa Zahanati na ukamilishaji wa maboma ya zahanati zaidi ya 1,000 Vituo vya afya zaidi ya 390 nchi nzima.

Aidha, Dkt. Dugange amesema Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha ujenzi wa hospitali ya kisasa ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe ambayo inatoa huduma za mionzi na huduma nyingine ambazo ziliwalazimu wananchi kuzifuata mikoa mingine.

Kadhalika, Dkt. Dugange amesema Mkoa wa Njombe ni moja kati ya mikoa 10 ya awali iliyopata shilingi bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya maalum ya wasichana kuanzia Kidato cha kwanza mpaka cha sita inayoendelea kujengwa mkoani hapo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!