Home Kitaifa CCM MAGU YAITIMISHA MAADHIMISHO YA MIAKA 46.

CCM MAGU YAITIMISHA MAADHIMISHO YA MIAKA 46.

CCM Wilaya ya Magu mkoani Mwanza imeishukuru serikali ya awamu ya sita ya inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutoa kiasi cha sh. bilioni 3.4 kujenga shule mpya ya wasichana ya bweni ya kimkoa katika mkoa wa Mwanza eneo la wilaya ya Magu ili kupata mazingira bora ya kusomea.

Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Enos Kalambo amesema uwepo wa shule mpya ya wasichana ya bweni ya kimkoa katika mkoa wa Mwanza eneo la wilaya ya Magu utapunguza umbali mrefu kwa wanafunzi hao sambamba na mimba za utotoni.

Chama cha mapinduzi wilaya ya Magu kimeitimisha maadhimisho ya miaka 46 kwa kuzaliwa chama hicho kwa kupanda miti katika kata ya Lutale, Ujenzi wa ofisi ya chama, kufanya usafi pamoja kushiriki ujenzi wa shule mpya ya wasichana kata Bujashi.

Kwa upande wake katibu wa chama hicho wa wilaya hiyo Moza Abdallah amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ujenzi wa shule hiyo huku akisema shule hiyo itakuwa mwarobaini wa kumaliza changamoto kubwa ya watoto wa kike katika mkoa wa Mwanza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!