Home Kitaifa TAASISI YA HAKIELIMU YATOA MAPENDEKEZO KWA SERIKALI ILI KUIMARISHA SHERIA YA MTOTO

TAASISI YA HAKIELIMU YATOA MAPENDEKEZO KWA SERIKALI ILI KUIMARISHA SHERIA YA MTOTO

Na Magreth Mbinga

Taasisi ya HakiElimu imeiomba Serikali ipitie upya sheria ,kanuni na miongozo kufuta vipengele vinavyo ruhusu matumizi ya adhabu ya viboko shuleni .

Hayo yamezungumzwa leo tarehe 26/01/2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa hakielimu Dkt. John Kalage wakati akizungumza na waandishi wa habari kutokana na tukio la adhabu ya kikatili waliyoipata wanafunzi wawili wa Shule ya msingi Kakanja iliyopo Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera.

Pia Dkt. Kalage amesema hakielimu inaipongeza Serikali kupitia Waziri wa Elimu ,sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda na uongozi w Mkoa wa Kagera kwa kuchukua hatua za haraka dhidi ya Mwalimu aliye husika na ukatili huo ikiwa ni pamoja na kumvua nafasi yake ya ualimu mkuu,kuunda tume ya kuchunguza tukio hilo ili hatua za kisheria ziweze kufuata.

“Mwaka 2016 katika Shule ya sekondari ya kutwa huko Mbeya ,walimu watatu kwa pamoja waliripotiwa kumpa adhabu ya viboko na ngumi mwanafunzi na kusababisha kulazaa Hospitali ,mwaka 2018 mwanafunzi Sperius Eradius wa Shule ya msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera alifariki kutokana na adhabu ya viboko kutoka kwa Mwalimu wake ,hii ni mifano ya matukio ya ukatili shuleni ambayo yabaahabihiana na hili na yameeipotiwa katika vyombo vya habari kwa nyakati tofauti” amesema Dk Kalage

Akiendelea kuzungumza Dk Kalage amesema katika utafiti uliofanywa na Shirika la HakiElimu mwaka 2020 takribani 87.9% ya watoto wa Shule waliripotiwa kufanyiwa ukatili wa kimwili huku 90% kati ya hao walisema ukatili wa kimwili waliofanyiwa ulitokana na adhabu za viboko zinazotolewa shuleni,katika utafiti huo 54.9%ya watoto walisema walimu wao na walezi wanatumia kupiga ngumi na makofi kama sehemu ya adhabu.

“Tanzania bado inakumbatia adhabu ya viboko kwa watoto na shuleni ,kwa mujibu wa mwongozo wa elimu juu ya adhabu ya viboko wa Mwaka 2002 Mwalimu Mkuu anaruhusiwa kutoa adhabu ya viboko kwa wanafunzi au kukasimisha jukumu hilo kwa Mwalimu mwingine ,mwongozo huu unapewa nguvu na sheria ya elimu ya mwaka 1978 na mabadiliko ya 2002 ” amesema Dk Kalage.

Aidha walimu wanasisitizwa kutumia mbinu mbada katika kusimamia nidhamu ya wanafunzi kwafano wanashauriwa kutumia vichocheo hasi ili kuwafanya wanafunzi wasiendelee na minendo ambayo haifai badala ya adhabu ikiwemo adhabu ya viboko.

“Kutokana na matukio haya HakiElimu tunatoa wito kwa Serikali kuchukua hatua ambazo zitakomesha kabisa matumizi ya adhabu za viboko shuleni na kuhimiza adhabu mbadala ambazo sio za kikatili ,rai yetu vipengele vya Aheria ya Elimu ya mwaka 1978 , Mwongozo wa elimu juu ya adhabu ya viboko wa Mwaka 2002 na sheria ya mtoto ya mwaka 2009 vipitiwe upya ili kukataza kabisa matumizi ya viboko shuleni na kuzuia adhabu nyingine ambazo zinaweza kutoa mwanya wa ukatili kwa watoto kufanyika” amesema Dk Kalage.

Sanjari na hayo Taasisi ya HakiElimu imetoa mapendekezo sambamba na mapitio ya sheria na miongozo ambapo mpango wa uanzishwaji wa Shule salama ufanyoke katika Shule zote,kutoa elimu kwa wanafunzi ,wazazi na jamii ili kuimarisha ulinzi,hatua Kali zichukuliwe dhidi ya watakaobainika kihusika na na vitendo vya ukatili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!