BONDIA wa Ngumi za kulipwa nchini Tanzania Mudy Pesa maarufu kama “Misumari ya zege” Amchimba Mkwala Mzito Mpinzani wake Aman Bariki Kutoka Gym Ya Uwanja Wa Kivita Kuelekea Kwenye Pambano La ” Kill Boxing Tour” linalotarajiwa kufanyika Febuari 25,2023 ukumbi wa YMCA Jijini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumza na Michuziblog leo Januari 26,2023 Mudy Pesa Amesema Mpinzani wake Atakutana na Chuma Kisicho Ogopa Ngumi Huku akiahidi Kumtwanga Katika Aridhi yake Mjini Moshi kwenye pambano Hilo.
“Nammiliki vizuri ‘Manchuga’ simuogopi wala simuhofii, mpinzani wangu nimemuona na ngumi zake hazina madhara nilishawahi kumshuhudia pambano lake uwanja wa Kinesi Jijini Dar es salaam hazijanitisha sijajua atanipiga ngumi gani mpaka niisikie.”
Hata hivyo amewaomba Mashabiki wa Mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani hiyo na kuwahakikishia mpinzani wake anampa kipigo mbele ya familia yake kutokana na matarajio ya pambano hilo kuwa zuri zaidi kutokana na maandalizi aliyojiandaa.
“Familia yake itashuhudia ugumu wa mtoto wao anavopata tabu katika utafutaji wa pesa, nimejipanga kwa ajili ya ”Manchuga” nitampiga ninavyotaka mimi kuna kitu nakitaka kwako”.
Hata hivyo kwa upande wa Kocha wake Fadhil Kambi amesema kuwa bondia Mudy pesa yupo vizuri siku zote lakini kutokana na kuwepo kwa pambano hilo wamekuwa wakimpa mazoezi mengi zaidi ili kumkabili mpinzani wake.
“Tutafanya mazoezi mara mbili yake kwa ajili ya pambano hilo na litavunja rekodi ya derby zote zilizofanyika tutakuwa fiti zaidi yake mbele ya Mkoani kwake.”
Mwisho.