Home Kitaifa RAIS DKT SAMIA AUMALIZA MGOGORO WA MIPAKA MBARALI ULIODUMU MIAKA 15

RAIS DKT SAMIA AUMALIZA MGOGORO WA MIPAKA MBARALI ULIODUMU MIAKA 15

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassam ameumaliza Mgogoro katika eneo la mbarali mkoani Mbeya uliodumu kwa miaka 15 kupitia tangazo la Serikali namba 28 ambao umefanyiwa marekebisho makubwa na kuwezesha kutoa hekta 74,000 kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji endelevu.

Kufuatia ridhaa hiyo, ranchi ya usangu pia imetolewa ndani ya eneo la hifadhi kupitia maboresho ya tangazo hilo ili kuruhusu shughuli za ufugaji endelevu.

Akizungumza wakati akitoa tangazo hilo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mheshimiwa Rais Dkt. Samia amefanya maamuzi hayo ili kuruhusu wananchi wa maeneo hayo kufanya shughuli endelevu za kilimo na ufugaji ili kujiletea maendeleo.

Ndugu zangu wanaKapunga, Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapenda sana, anatamani kuona mkipata maendeleo kupitia shughuli zenu hizi, uamuzi wake huu ni ishara ya upendo wake wa dhati kwenu

WANANCHI wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwa kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 15 na hivyo kuwawezesha kuendelea kufanya shughuli zao za ufugaji na kilimo kwa uhuru na amani.

Wamesema kumalizika kwa mgogoro huo ambao ulihusisha wakazi wa wilaya hiyo wanaoendesha shughuli za ufugaji na kilimo katika eneo la Bonde la Usangu dhidi ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Tunamshukuru mama yetu, Mheshimiwa Rais Samia kwa uamuzi mkubwa alioufanya wa kuboresha GN 28, sasa tutalima kwa uhuru na tutaongeza uzalishaji kwa sababu awali tulikuwa tunalima kwa wasiwasi,” Amesema Elibauti Mwinuka mkulima katika kata ya Itamboleo wilayani Mbarali.

Kwa upande wake, Anle Kifute ambaye ni mkulima katika kijiji cha Kapunga amesema amefurahishwa na kauli ya Serikali ambayo inakwenda kuwaondolea migogoro katika maeneo yao na hivyo wataweza kuendesha shughuli zao bila ya usumbufu wa aina yoyote.

Naye, Mwenekiti wa Wafugaji katika ranchi ya Matebele-Madunguru, Lokordu Siloma amesema amefarijika kwa uamuzi huo wa Serikali pamoja na elimu ya ufugaji wa kisasa na wenye tija waliyopatiwa ambayo inakwenda kuongeza mnyororo wa thamani.

Kadhalika amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi na sasa wanakwenda kufuga kwa uhuru na kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa. “Awali watu wenye uwezo walikuwa wanavamia maeneo ya ranchi na kuendesha shughuli za kilimo lakini kwa kauli hii wafugaji tutaachiwa ranchi zetu tulishe mifugo yetu. Tunaishukuru sana Serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!