Home Kitaifa KOROGWE YATOA MILIONI 97 KWA VIKUNDI 16

KOROGWE YATOA MILIONI 97 KWA VIKUNDI 16

Na Boniface Gideon, TANGA

HALMASHAURI ya Mji Korogwe (Korogwe TC) mkoani Tanga imetoa mikopo yenye thamani ya sh. milioni 97 kwa vikundi 16 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2022. Ni asilimia kumi ya Mapato ya Ndani pamoja na marejesho yatokanayo na mkopo.

Wakati Halmashauri hiyo inakopesha fedha hiyo sh. milioni 97, tayari ilishatoa sh. 568,204,502 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi 2021/2022 kwa vikundi 166 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ambapo katika fedha hizo, sh. 408,904,502 ni za asilimia 10, na sh. milioni 159.3 ni marejesho.

Hayo yalisemwa juzi jana na Kaimu Ofisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Korogwe Rehema Letara, kwenye hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa Soko la Manundu mjini Korogwe, na mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Dkt. Alfred Kimea.

Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi 2021/2022 halmashauri imetoa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu yenye jumla ya sh 568,204,502. Kati ya hizo, asilimia 10 ni sh. 408,904,502, na marejesho sh. 159,300,000. Fedha hizi zimekopesha vikundi 166. Aidha, vikundi vya wanawake vilivyokopeshwa ni 90 na walipata sh. 314,231,815 na wamerejesha sh. 122,072,687, vijana vikundi 55 sh. 236,422,730 na wamerejesha sh. milioni 74.7, na watu wenye ulemavu 21 mkopo wa sh. milioni 131.9 na wamerejesha sh. 53,534,300″.

“Katika kipindi cha Julai hadi Desemba, halmashauri imetoa mikopo yenye thamani ya sh. milioni 97 kwa vikundi 16 Fedha hizi ni asilimia kumi ya Mapato ya Ndani pamoja na marejesho yatokanayo na mkopo” alisema Letara.

Dkt. Kimea alivitaka vikundi hivyo kutumia fursa ya mikopo kutoka Halmashauri ili viweze kujikwamua kiuchumi, huku akivitaka vikundi hivyo kurudisha mikopo hiyo kwa wakati muafaka ili watu wengine waweze kukopa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!