Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Daniel Chongolo ametoa onyo kwa makatibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kujihusisha na makundi ya wagombea katika uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama na jumuiya zake.
Ameeleza hayo akiwa mgeni rasmi katika kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania Makao Makuu ya Chama Dodoma jana Jumatano tarehe 15 Juni, 2022.
“Narudia natoa onyo kwa makatibu wote nchini, ninyi ni wakurugenzi wa uchaguzi, sitamani wala nisingependa kuona mnalichukulia suala hili la uchaguzi kishabiki kwa kutengeneza wagombea, nawaasa, kazi ni nzuri ukiikosa lakini ni mbaya sana ukiwa nayo.” aliisitiza