Na. Mercy Maimu :
Mamlaka ya bima nchini imewataka wazazi na walezi kote nchini kuelewa umuhimu wa kuwakatia bima za maisha watoto ambazo zitawasaidia katika kuyafikia malengo na kutimiza ndoto zao walizojiwekea.
Wito huo umetolewa na kamishna wa bima nchini Dr. Baghayo Saqware katika hafla ya kuwatunuku zawadi washindi watano milioni sita na elfu sabini tano kwa kila mmoja ambao ni wanafunzi walioshiriki katika shindano la uchoraji wa shule za jimbo ambayo imeandaliwa na Jubilee Insuarance Leo, Jijini Dar es Salaam.
Amesema bima za maisha kwa watoto zina umuhimu mkubwa sana hususani katika kusaidia kutoa mafao kwa ajili ya ada kwa maendeleo elimu kwa ujumla.
“Bima hizi zina umuhimu katika maisha ya watoto ikiwa ni pamoja kusaidia watoto katika maendeleo Yao ya Elimu na hata maisha kiujumla”. amesema Saqware
Aidha amesema soko la Bima kwa sasa liko salama na muamuko wa watu kutumia bima za maisha umeongezeka mpaka kufikia asilimia 11 ikiwa ni hatua kubwa ya watanzania wengi kuona umuhimu wa Bima hizo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jubilee Life Insuarance Helena Mzena amesema katika kuendelea kuimarisha Elimu nchini si kuwapa bima za maisha wanafunzi hao tu bali pia wamefanya marekebisho katika shule mbalimbali zenye changamoto kwa kujenga madarasa ,vyoo na nyumba za walimu pamoja na kufanya shindano la uchoraji kwa wanafunzi.
“Katika kuadhimisha miaka 80 ya
utoaji huduma, Jubilee Holdings ilitekeleza Shughuli mbali mbali za kujitolea
kwenye jamii ambazo zilijumuisha ukarabati wa Shule mbalimbali nchini”. amesema Mzena
Uwepo wa bima nchini ni kulinda maslahi ya biashara ,watu binafsi ,taasisi na kampuni kwa kutoa huduma bora zinazolenga kukidhi mahitaji yao ya bima za maisha, afya, moto na Magari.
Washindi hao Salma Musa,Atupele Westoni Ezrael,Petro Mwakyeme,ibrahim Miraji na khadija Mohamed.