Home Kitaifa Pochi la Mama kusajili wanafunzi 9226 kidato cha kwanza 2023 Kwimba

Pochi la Mama kusajili wanafunzi 9226 kidato cha kwanza 2023 Kwimba

Mradi wa Ujenzi wa Madarasa kwa ajili ya mapokezi ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023 (Pochi la Mama) wafanikisha kuchaguliwa watoto 9226 kwa wakati mmoja kujiunga na kidato cha kwanza mapema juma lijalo wilayani Kwimba Mkoani Mwanza kutokana na Ujenzi wa madarasa 112 kwa Bilioni 2 na Milioni 240.

Akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa ukamilishaji wa Madarasa hayo uliofanyika katika Shule ya Sekondari Nyamilama ambapo yamejengwa Madarasa 12 kwa Milioni 240, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Adam Malima amewapongeza Viongozi wa wilaya hiyo kwa ushirikiano uliofanikisha zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya elimu nchini.

“Najua mafanikio ya Ujenzi huu ni ishara ya kuwa kila mmoja amefanya wajibu wake maana madarasa 112 sio mchezo mdogo kwani mama Samia kuleta fedha nyingi ni jambo moja lakini kutekeleza kilichoagizwa ni suala lingine na kwakweli nawapongeza wote kwa kuhakikisha jambo hili linafanikisha.” Amesisitiza Mhe. Malima.

Aidha, ametoa rai kwa wanafunzi kuhakikisha wanaweka bidii kwenye Elimu ili uboreshaji wa Miundombinu na samani kwenye shule za Sekondari uendane na ukuzaji wa ufauli hasa kwa masomo ya Sayansi na amebainisha kuwa wanafunzi wanaosoma mjini wako sawa na wanaosoma shule za vijijini hivyo wasijione wanyonge.

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe. Johari Samizi ametumia wasaa huo kuwapongeza Viongozi na wananchi wote walioshiriki kufanikisha Ujenzi na amebainisha kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kufanikisha uboreshaji wa huduma za kijamii wilayani humo kwani amepeleka fedha nyingi kwenye Sekta za Maji, Barabara na Afya.

“Rais Samia wakati anaingia madarakani alikuta wilaya hii haina umeme kwenye vijiji vyote lakini kwenye uongozi wake tumepata umeme kwenye Vijiji vyote na alikuta bajeti ya Ujenzi wa Barabara vijijini ilikua Milioni 700 lakini hivi sasa tumefikia Bilioni 3.6, ndio maana wanakwimba tunampenda.” Mhe. Mageni Kasalari Mbunge wa Sumve, kwa niaba ya Mbunge wa Kwimba.

Akitoa taarifa ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Happiness Msanga mesema mwezi Oktoba 2022 walipokea Shilingi Bilioni 2.24 kujenga Madarasa 112 kwenye shule za Sekondari 33 na kwamba tayari Ujenzi umekamilika na wanafunzi wapatao 9226 watasajiriwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 kwa wakati mmoja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!