Home Kitaifa WATUMISHI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

WATUMISHI WATAKIWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya amewataka watumishi wote kutoa huduma bora kwa wanachi ili kutimiza adhima ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Dkt. Godwin Oloyce Mollel amesema hayo leo (Januari 03,2023) katika ziara yake aliyoifanya Hospitali ya Wilaya ya Ubungo – Mkoa wa Dar es Salaam.

hatutakuwa tumefikia adhima ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan kama yule anayetumia wa mwisho ambaye ni mwananchi hajapata huduma bora” amesema Dkt Mollel

Aidha Dkt Mollel ameipongeza wilaya ya ubungo kwa ushirikiano walionao, “kwenye ubora wa huduma ya afya ni hichi ambacho nyie mmekifanya tunashirikiana wote kwa pamoja” amesema

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri D. James amesema ni wilaya yenye watu wengi, zipo sekta nyngi zimewekezwa hapa, “ni lazima wilaya hii iwe na huduma bora sana za Afya,

Zahanati,Vituo vya Afya zinajengwa na Hospitali ya wilaya inaimarishwa kwa kasi ili kuhakikisha swala la afya kwa wananchi wetu linapatikana na kuhakikisha huduma bora za afya na huduma za karibu ili Mgonjwa asitembee umbali mrefu” amesema

Kwa upande wake katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya ya ubungo Juma Kinshashu ameishukuru Serikali kwa kujenga Hospitali ya Wilaya kwani itaenda kumaliza kabisa tatizo la Huduma za Afya kwa Wanachi wa Ubungo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!