Home Michezo IBRAHIM MAFIA KUZICHAPA LEO NA JUMA FUNDI KUWANIA MKANDA TPBRC.

IBRAHIM MAFIA KUZICHAPA LEO NA JUMA FUNDI KUWANIA MKANDA TPBRC.

Na Boniface Gideon, TANGA

BONDIA Ibrahim Mafia wa Jijini Tanga aliye chini ya usimamizi wa kampuni ya Mafia Boxing Promotion Leo anatarajiwa kupanda ulingoni kuwania Ubingwa wa TPBRC katika uwanja wa mkwakwani Jijini Tanga kwa kumkaribisha Bondia Juma Fundi kutoka Dar esalaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati Wa zoezi la upimaji uzito, Meneja wa kampuni ya Mafia Boxing Promotion ambao ndio Waandaji wa pambano Hilo Plantan shabaha alisema kampuni hiyo iliamua kuleta pambano Hilo Jijini Tanga kwa lengo la kuamsha hamasa ya ngumi Jijini Tanga,

Tumeamua kuleta pambano hili hapa Tanga kwa kuzingatia baadhi ya Mambo ikiwamo kuhamasisha mchezo wa ngumi mkoani Tanga lakini pia ni Sehemu ya kurudisha Shukrani kwa Wana Tanga kutokana na Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion anatoka Tanga na Wananchi wa Tanga wamekuwa mstari wa mbele kutuunga mkono hivyo tumeona turudishe Shukrani zetu na ndio Mana hata viingilio tumeweka Sh.2,000/5,000 ili kumwezesha kila mtu kupata furasa ya kuingia” Alisisitiza Shabaha

Alisema kampuni hiyo itaendelea kuandaa mapambano mengine ikiwemo pambano la ngumi Februari 4 mwaka huu ambapo Mabondia akiwamo Salum Mtango atapanda ulingoni na mwezi Machi na yote yafanyika Jijini Tanga,

Tutaendelea kuandaa mapambano mengine ikiwemo pambano la mwezi Februari 4 mwaka huu na mwezi Machi tutakuwa na pambano, yote haya tutawapa ratiba kamili lakini tunategemea kuandaa mapambano mengi zaidi lengo ni kuupaisha mchezo wa ngumi Nchini mpaka tumpate Bondia mwenye nyota 5 Nchini “ Alisema Shabaha

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!