Home Kitaifa VIONGOZI WOTE WA KATA NA MATAWI WATAKIWA KUFANYA KAZI NA KUACHANA NA...

VIONGOZI WOTE WA KATA NA MATAWI WATAKIWA KUFANYA KAZI NA KUACHANA NA MAJUNGU NA FITNA

Na ZIANA BAKARI

VIONGOZI wa kata na matawi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Ubungo, wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu na kuachana na majungu na fitna zisizokuwa na tija wala malengo katika jumuiya yao ambayo haitawaletea maendeleo ya aina yoyote.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Shadrack Makangula, alipokuwa anaongoza kikao cha baraza katika kata ya Msigani Dar es Salaam, juzi, baraza hilo lilikuwa la uchaguzi wa wajumbe wa kamati ya utekelezaji na Dira ya muelekeo wa jumuiya yao.

Alisema kiongozi yoyote anapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa wale anaowaongoza hivyo ni vyema kwa kila kiongozi kuwa na uadilifu katika kazi na kuzingatia utaratibu unaopaswa kufanywa na sivyo kufanya vitu vingine vya utofauti.

Nawashukuru wajumbe wa baraza kwa kufanya uchaguzi kwa amani, tumefanikiwa kupata washindi watatu ambao ni Kazumba Charles, Kelvin Kennedy na Noela Joachim.

Wajumbe hawa wataenda kuunda safu timilufu ya kamati ya utoke ya UVCCM katika Wilaya yetu, kuanzia mwaka 2022 hadi 2027, niwaombe kufanya kazi vizuri tuweze kufikisha jumuiya yetu mbali tuweze kunufaika na matunda yetu katika Chama,“alisema Makalunga.

Aidha, aliwaomba wajumbe hao waliochaguliwa kutoa ushirikiano katika viongozi na wanachama wengine kwani umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu hivyo endapo watadumisha umoja wao na ushirikiano basi jumuiya hiyo itasimama kwa imara na kuleta maendeleo lukuki.

Sasa tumetimia, hivyo ni wajibu wetu sote tuwe na ushirikiano kwa pamoja, kila mmoja katika eneo lake aende atekeleze kile kinachopaswa kutekelezeka kwa maslahi ya jumuiya yetu ya UVCCM na Chama chetu kiujumla bila kusahau kwenda kushawishi vijana wengine kujiunga na Chama chetu.

Lengo letu ni kuleta matokeo na kuhakikisha tunafanikiwa katika jumuiya yetu na Chama chetu, ilituweze kufanya vyema katika chaguzi za usoni za kiserikali 2024 na 2025 tunaibuka na ushindi wa kishindo,”alisema Makangula.

Mbali na hayo, Baraza la UVCCM Wilayani hapo, limemthibitisha Ezekiel Obote, kuwa katibu wa hamasa na chipukizi wa Wilaya hiyo, lakini kila baada ya miezi mitatu kutakuwa na utaratibu wa kukutana na viongozi kuweka ukaribu na kujua changamoto wanazokumbana nazo kwani matarajio yao ni kujenga jumuiya imara na shirikishi.

Viongozi wote wa kata na matawi wahakikishe wanatembelea miradi iliyopo katika maeneo yao, kuona utekelezaji upoje na hatua ya miradi ilipofikia, sisi ni walinzi wa Chama chetu hivyo ni wajibu wetu kukagua miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani na kuisimimia vyema ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi,“alisema Makangula.

Kwa Upande wao, wajumbe waliochaguliwa walimpongeza Mwenyekiti huyo na kuahidi kuwa, watatekeleza vyema majukumu hayo waliyopewa na kuhakikisha wanailetea maendeleo jumuiya hiyo.

Tutahakikisha tutaleta matunda bora katika jumuiya yetu, kitu cha muhimu tunaomba viongozi wetu watupe ushirikiano katika kazi tutakazokuwa tunazifanya kwa kipindi kuanzia mwaka 2022 hadi 2027,“walisema.

Naye, Katibu hamasa na Chipukizi wa Wilaya hiyo, Ezekiel Obote alitoa shukran za dhati kwa viongozi hao kumchagua na kujipatia nafasi hiyo na kuahidi kutekeleza vyema majukumu yake na kuleta maendeleo ya Chama hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!