MAKAMU Mkuu wa Chuo, William Anangisye, amewataka wanafunzi wa Chuo kikuu Cha Dar es Salaam, kuwa wazi kwa viongozi wao na watu wao wa karibu kuweza kusaidiia jinsi ya kuepukana na mawazo hayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaan katika maadhimisho ya Siku ya afya ya akili yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es salamu, Dkt Anangisye alisema ni vyema kwa kila mwanafunzi kuwa wakweli kwa viongozi wao na watu wa karibu ili kuwasaidia kutatua matatizo mbalimbali kama kimaisha, kiuchumi.
Alisema suala la afya akili inapaswa kupewa kipaumbele katika jamii kwa lengo la kujenga jamii yenye furaha kutokana na kauli mbiu inayosema ‘Afya ya akili kipaumbele kwa wote.
“Natoa pongezi kwa uongozi wa chuo kwa kuandaa kongamano la awamu ya pili ya afya ya akili katika taasisi ya elimu ya juu, niwashukuru Ofisi ya PFA kwa kutenga fedha kea lengo la kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji.
“Niwashauri wanafunzi kujitahidi kuwa wawazi kwa viongozi wenu, lakini wanafunzi wanapaswa kuwa na nafasi ya kusikilizwa kwa lengo la kutambua changamoto wanazopata,”alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha ushauri na unasihi kutoka chuo cha Udsm, Dkt. Bernadetha Rushahu, alisema afya duni ya akili husababisha umasikini na msongo wa mawazo hupelekea watu kuwa na tamaduni za kunywa vinywaji hatari hususani vilevi na kushindwa kujiamini.
“Jamii inapaswa kujitofautisha na matatizo na visababishi vya matatizo, ni vyema tutambue jinsi ya kukabiliana na matatizo na tuwe wazi kwa wenzetu kwa kuchangia matatizo yako kwa rafiki yako wa karibu unayemuamini,“alisema Dkt. Rushahu